KWANI BIBLIA INASEMAJE KUHUSU UTOAJI WA SADAKA ZAKO!!!!

| Makala

KWANI BIBLIA INASEMAJE KUHUSU UTOAJI WA SADAKA ZAKO!!!!

Na kwanini hauoni matokeo ya sadaka unazozitoa madabahuni!!

Maisha ya watu wengi sana,na huenda kwa asilimia zote hata wewe umekamatwa kwenye hili eneo, maisha yako yamekwama kwa sababu ya kushindwa kumtolea Mungu sadaka anazozitaka kwako.na wakati mwingine unatoa ila unatoa kwa muda unaotaka wewe na kiwango unachokitaka wewe.

Mungu anapoitaka sadaka yake kutoka kwako anazingatia haya mambo matatu ya msingi sana ambayo inakupasa na wewe kama mtoaji uwe makini kuyafahamu mambo haya.

=> iko hivi mtu wa Mungu, Suala la muda kiroho ni suala muhimu sana kuliko maelezo, na Mungu anapotaka umtolee sadaka zako huwa anakusemesha ndani ya moyo wako kwa majira maalum kupitia mtumishi wake anayekufundisha au Roho Mtakatifu. Na kwanini uzingatie muda wa kutoa? Kwa sababu Mungu ameona mazingira ya yeye kukusaidia majoira fulani na anataka aunganishe moyo wako uliobeba hiyo sadaka ili akusaidie.

By the way, kinachobeba sadaka ni moyo na sio mkono wako, na ndio maana kwenye kitabu cha Kut 25:1

BWANA akanena na Musa, akamwambia, Waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu. 

Mikono huwakilisha utoaji wa sadaka ila sadaka inabebwa na moyo wa mtoaji wa hiyo sadaka.

Ndio maana biblia inatuambia katika kitabu cha Luka 12:34 

Pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako.

Ikitokea umepata maelekezo ya kutoa sadaka madhabahuni pa Bwana na ukapuuzia suala la muda na wewe ukataka utoe kwa muda unaoutaka wewe na sio muda wa Mungu, hiyo sadaka haitafaa tena na hakuna matokeo utakayoyavuna kwa utoaji wako.

Leo hii maisha yako yamekwama sio kwa sababu hautoi sadaka zako, Sadaka unatoa ila unatoa kwa kujiamulia wewe utoe muda gani na majira gani…

Mungu anapoitaka sadaka yako ili akusaidie,haoni kitu kwahiyo anakuacha na matatizo yako mpaka siku utakaposhtuka na kuanza kutoa kwa muda sahihi….

Usicheleweshe sadaka yako ya zaka

Usicheleweshe sadaka yako ya malimbuko

Usicheleweshe sadaka yako ya shukrani 

Usicheleweshe sadaka yako ya mbegu 

Na sadaka zingine zote utakazoelekezwa kuachilia madhabahuni.

Kitabu cha Mal 2:3 Mungu anaongea maneno magumu sana hapa…..

“Angalieni, nitaikemea mbegu kwa ajili yenu, nami nitapaka nyuso zenu mavi, naam, mavi ya sadaka zenu; nanyi mtaondolewa pamoja nayo”

“Faida ya utoaji ipo kwa mtoaji”

Tupatane sehemu ya pili ili nikuonyeshe point ya pili ambayo unapaswa sana kuizingatia wakati unamtolea Mungu sadaka zako….maana hii ndio sababu kubwa wengi mnalalamika kwanini hamuoni matokeo ya sadaka zenu.

Hagai 1:6-7 

Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka. BWANA wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.

Pastor Innocent Mashauri

Madhabahu ya SIRI ZA BIBLIA

Maarifa ya ki-Mungu

+255 758 708804

 


 SADAKA